MADHARA YA TEZI DUME
(COMPLICATIONS)
Kushindwa kukojoa. (urinary retention )
UTI :Ukishindwa kutoa mkojo wote kwenye bladder unakaribisha Maambukizi kwenye Njia ya mkojo.
Uharibifu wa kibofu (bladder damaged) kibofu kisipomaliza mkojo kitatanuka na kuwa dhaifu (stretching and weaken)
matokeo yake kuta za misuli haziwezi kujikunja kuusukuma mkojo nje. na kufanya mkojo ubaki kwenye kibofu.
Mawe ya kwenye kibofu (Bladder stones) hili ni tatizo linalotokea a na kushindwa kumaliza mkojo wote kwenye kibofu.
Uharibu wa Figo ( kidney damage ):shinikizo ( pressure ) kubwa kwenye kibofu kwa kushindwa kuusukuma nje mkojo huaribu Figo au kibofu kupata Maambukizi yatakayofika kwenye Figo.