UGONJWA WA KISUKARI

DIABETES MELLITUS

Kisukari ni ugonjwa ambao humsababishia mtu kuwa na kiwango kikubwa cha sukari katika damu
na kushindwa kuitumia sukari hiyo ipasavyo ili kumpa nguvu.
na hivyo sukari hiyo kutoka nje ya mwili wa mgonjwa kupitia njia ya mkojo.
Ugonjwa huu pia huitwa Diabetes Mellitus, maneno yanayotokana na kigiriki na kilatini.
Diabetes linatokana na kigiriki likimaanisha kijibomba kinachonyonya maji na mellitus linatokana na neno la kilatini

“ Mel ”

lenye maana ya asali, hivyo diabetes mellitus ni

“ kunyonya maji yenye utamu kama asali”

Baada ya madaktari wa enzi hizo kugundua kuwa mkojo na damu ya mgonjwa wa kisukari vilikuwa na glucose kwa wingi sana.
Wachina wa zamani nao waligundua kuwa mchwa walijaa kwa kwingi kwenye eneo la mkojo wa mtu mwenye kisukari kutokana na mkojo huo kuwa mtamu na wakatoa neno

 “ Sweet Urine Disease ”

Ugonjwa wa kutoa mkojo mtamu.

TATIZO LA KISUKARI

Kisukari (Diabetes Mellitus) ni kundi la ugonjwa ambao una athiri mwenendo wa Matumizi ya sukari ya kwenye damu (glucose)
Glucose ni chanzo kikuu na muhimu cha nishati (energy) kwa ajili ya cell ambazo hutengeneza misuli na tissue.
Pia ni chanzo kikuu cha kulisha ubongo (brain)
Kinachosababisha hasa Kisukari ( diabetes ) hutegemea na chanzo.
Bila kuangalia aina ya kisukari mtu alichonacho tatizo hukupelekea kuwa na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu ( excess sugar )
Sukari ya ziada kwenye damu hupelekea tatizo kubwa sana la afya (serious health problems)

AINA KUU ZA KISUKARI

Diabetes Type 1

Mwili kuto zalisha insulini (insulin)  ya kutosha

Aina ya pili ni Diabetes Type 2

Mwili kuzalisha insulini (insulin)  lakini kutoitumia vizuri mwilini

Aina ya tatu ni  Gestational Diabetes (kisukari cha ujauzito)

Hali ya muda katika ujauzito

Hali ya Kisukari Sugu ( Chronic Diabetes)

Hii huusisha na :

-Kisukari aina 1( diabetes type 1 )
-Kisukari aina ya 2 (diabetes type 2)

Hali zingine za kuelekea kwenye Kisukari huusisha:

-Kisukari cha mwanzo (Prediabetes)
-Kisukari cha ujauzito (gestational diabetes)
Kisukari cha mwanzo Hutokea wakati kiwango cha sukari  kwenye damu ni kikubwa kuliko kawaida.
Lakini sukari kwenye damu haitoshelezi kuitwa Kisukari (diabetes).
Kisukari cha mwanzo (prediabetes) hupelekea mtu kupata Kisukari kama Hatua hazikuchukuliwa kuzuia.
Kisukari cha ujauzito (gestational diabetes) hutokea wakati wa Ujauzito (pregnancy).
Kinaweza kutoendelea Baada ya Mtoto kuzaliwa au mama kujifunga.

DALILI ZA KISUKARI (SYMPTOMS)

Dalili za Kisukari hutegemea kiasi gani cha sukari kwenye damu ipo.
Baadhi ya watu hasa wenye prediabetes, gestational na type 2 diabetes, anaweza was iwe na dalili.
Kisukari Type 1, dalili zake huja haraka sana na zinaumiza (more severe)

BAADHI YA DALILI ZA KISUKARI DIABETES TYPE 1 na 2 

Ketones ni mabaki yanayotokana na kuvunjavunja kwa misuli na mafuta kunakotokea wakati Hakuna insulin

SABABU ZA KISUKARI (CAUSES)

Kuelewa Kisukari ni vyema na muhimu Kuelewa jinsi gani mwili hutumia glucose
JINSI GANI INSULIN HUFANYA KAZI

KAZI YA GLUCOSE NI NINI

Glucose ni sukari kwenye damu na ni chanzo cha nishati kwenye cell ambazo hutengeneza  misuli na tishu (muscles na tissues)
Glucose Hupatikana kutoka kwenye vyanzo viwili (2)
(1) Chakula (Food)
(2) INI (Liver)
Glucose huzama kwenye mzunguko wa damu, ambapo huingia kwenye cell kwa msaada wa insulin.
INI (Liver) hutunza na kutengeneza glucose, Wakati kiwango cha glucose kikiwa chini yaani Ukiwa hujala kitu,
INI huvunjavunja sukari iliyotunzwa (glycogen) kuwa glucose.
Hii Hufanya kiwango cha glucose kuwa kinachotakiwa (typical range)
Kisababishi hasa ya aina za Kisukari huwa haijulikani, vyovyote hivyo sukari hujijenga kwenye mzunguko wa damu.
Kwa sababu kongosho (pancreas) haitoi insulin ya kutosha (enough insulin)
Aina zote za Kisukari yaani type 1 na type 2 husababisha na mkusanyiko wa sababu za

VIHATARISHI VYA KISUKARI (RISK FACTORS)

Vihatarishi vya Kisukari hutegemea na aina ya kisukari.
Historia ya Familia huwepo kwenye aina zote za Kisukari.
Sababu za Kimazingira ( environmental factors )na za kijographia Huongeza uhatari wa Kisukari type 1
Wakati mwingine watu wenye Kisukari Type 1 huwa Wana tatizo kwenye mfumo wa  Kinga ya kisukari( auto antibodies).
Kama una hizi auto antibodies, unakuwa kwenye hatari zaidi kupata Kisukari Type 1.
Lakini sio lazima Ukiwa pia na hizi auto antibodies kuwa na Kisukari.
Rangi na Koo( Race na ethnicity) huiamsha uwezekano wakubwa na Kisukari Type 2.
Ingawa haijulikani kwa nini, watu weusi (black), Hispanic na wahindi Wekundu a waasia wako kwenye uhatari mkubwa.
Kisukari cah mwanzo ( prediabetes ) na Kisukari cha ujauzito ( pregnancy ) ni visukari vya kawaida kwa watu wenye uzito mkubwa ( overweight au obesity)

MADHARA YA KISUKARI (COMPLICATIONS)

Madhara ya kisukari hujijenga pole pole kwa muda mrefu.
Unapokuwa na Kisukari kwa muda mrefu bila kukitibu na kudhibiti sukari unakuwa kwenye hatari kubwa ya madhara.
Madhara ya kisukari huwa ni ya kudumu au kukupa kilema cha maisha (life threatening)
Dalili za Kisukari cha mwanzo hupelekea kupata Kisukari halisi.

Madhara kwa jumla ni haya:

Figo huwa na vimishipa vya damu (million of tiny blood vessels) Zinazoitwa glomeri
Glomeruli kazi yake kubwa ni kuchuja Uchafu kwenye damu (filtration)
Kisukari huaribu Huu mfumo ngumu wa uchujaji.

KUZUIA AU KUJIKINGA NA KISUKARI

Ni ngumu kuzuia Kisukari Type 1 lakini
Kisukari Unaweza kukizua kwa
Pata muda angalau wa Nusu saa wa kufanya mazoezi  ya kawaida (aerobic activities)
Punguza uzito wa ziada (lose excess pound)
Kupoteza angalau 7% ya uzito wako Mfano kama una kilo 90.7 punguza kilo 7 utapunguza hatari ya diabetes.
Lakini usijaribu kupunguza uzito wakati wa Ujauzito.
Naitwa DR. Juma Mwesigwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Huheso Fm Redio iliyopo Kahama Shinyanga Tanzania
Pia ni Mkurugenzi wa Shirika la HUHESO Foundation lenye makao makuu mkoani Shinyanga
Ni mtaalamu wa tiba lishe zaidi ya miaka mitano (5).
Msambazaji wa bidhaa zinazotibu magonjwa mbalimbali yasiyo ambukiza.
Kwa kutumia bidhaa hizi za BF SUMA zimekuwa na matokeo makubwa sana kwa wanaozitumia na kubadili Maisha yao.